WASHTAKIWA WA UGAIDI MOMBASA WASHINDWA KUELEWA TAFSIRI

Washukiwa wa Ugaidi wakiwa Kizimbani Mombasa
Kesi dhidi ya wanawake watatu walioshukiwa kuhusika katika shambulio dhidi ya kituo kimoja cha polisi katika mji wa bandarini wa Mombasa nchini Kenya mwishoni mwa juma, ilishindwa kufanyika kutokana na matatizo ya mawasiliano.
Mmoja wa washukiwa hafahamu kabisa Kiingereza au Kiswahili.
Shukri Ali, ambaye ni mlemavu wa kutosikia, hakujibu lolote hata baada ya mfasiri wa ishara aliyeletwa mahakamani kumsaidia kuelewa kesi dhidi yake.
Mtafsiri wa lugha ya Kisomali pia alikuwa mahakamani ili kuwasaidia washukiwa wawili, Saida Ali na Naima Mohamed Ali, ambao hawana uwezo wa kufahamu Kiingereza.
Shukri Ali, Saida Ali na Naima Mohamed Ali mahakamani, Mombasa
Jaji Emmanuel Mutunga, aliamuru Shukri Ali, kupelekwa hadi katika wachunguzi maalum wa kimatibabu, katika hospitali ya kitaifa ya Coast General.
Wanawake hao watatu, ambao bado wanazuiliwa pia watachunguzwa na madaktari.
Wanashtakiwa kwa kosa la kuwapa hifadhi wanawake watatu wanaodaiwa kuunga mkono kundi la Islamic State, ambao waliuwawa pale walipojaribu kushambulia kituo cyha polisi cha Mombasa siku ya Jumapili iliyopita.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 21, wakati ripoti ya kimatibabu itakapowasilishwa mahakamani.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.