EDWARD LOWASSA AMPONGEZA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

Image result for lowassa

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa kuondoa urasimu katika taasisi za serikali na kusema hiyo itasaidia kurejesha utendaji kazi kwa ufanisi.

Lowassa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mtangazaji wa BBC, John Nene nchi Kenya ambapo alisema urasimu umepungua na hili amejitahiidi lakini kuna mambo baadhi hayako vizuri.

Lowassa hakuwa tayari kusema ni mambo gani haswa hayakua yakienda sawa lakini alimkosoa Rais Magufuli kwa kile alichodaiwa kuwa analeta dalili za udikteta.

Amekosoa pia uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kupiga marufuku maandamano, mikutano na vikao vya ndani vya vyama siasa huku vyombo vya habari vikifungiwa na wale wote wanamkosoa wakifikishwa mahakamani.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.