DIAMOND | AY | DJ D OMMY | HARMONIZE | WAMETULETEA WATANZANIA USHINDI HUU KWENYE TUZO ZA AEA - USA
Wakati Watanzania wengi macho na masikio yetu tukiwa tumeyaelekeza kwenye tuzo za MTVMama ambazo zimetolewa Afrika Kusini lakini usiku huo huo wa Oct 22 nchini Marekani kulikua pia kukitolewa tuzo ambazo Watanzania pia walishiriki.
Tuzo ambazo zilitolewa marekani zinajulikana kama African Entertainment Awards Usa 2016 (AEA) kitu kizuri na kikubwa ni kwamba Watanzania wameshinda pia kwenye tuzo hizo kwenye baadhi ya vipengele.
Kipengele cha Msanii bora anaechipukia kashinda Harmonize, Kipengele cha wimbo bora wa kushirikiana/kushirikishwa umeshinda wimbo wa Zigo wa AY, Kipengele cha DJ Bora ni Dj D Ommy na msanii bora wa kiume kashinda Diamond Platnumz.
No comments:
Post a Comment