DOGOO JANJA ATANGAZA KUOA HIVI KARIBUNI.... ATAKI UKAPERA
Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja ametangaza rasmi kuwa ana mpango wa kuoa hivi karibuni.
Rapper huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Kidebe’ amesema amempata mtu sahihi ambaye anaweza kufunga naye ndoa nakuachana na ukapera.
“Yah ni kweli nataka kuoa muda si mrefu nitavuta jiko hivyo siwezi kusema ni lini ila suala hilo lipo kwenye mchakato” Dogo Janja alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Kwa upande wa Madee ambaye ni mlezi wa Dogo Janja kimuziki na katika maisha ya kila siku alisema kuwa kitendo cha Dogo Janja kutaka kuoa kabla yake itakuwa kama dharau hivyo anapaswa kusikilizia kwanza mpaka yeye afanye mambo kwanza ndipo na yeye atangaze.
“Ha ha ha ha Dogo Janja kuoa kabla yangu itakuwa kama dharau aiseee anapaswa kusubiri kwanza mimi nifanikishe jambo hilo ndiyo yeye afuate” alisema Madee
No comments:
Post a Comment