MAAMUZI YA SERIKALI BAADA YA KUONA ILE VIDEO YA MWANAFUNZI AKICHANGIWA NA WALIMU WA " FIELD " MBEYA DAY
Tukio linaloonyesha mwanafunzi wa shule ya sekondari Mbeya Day akipigwa na baadhi ya walimu huku wakimchangia kwa pamoja, tumeona baadhi ya viongozi wa kiserikali wakitumia nafasi hiyo pia kulaani tukio hilo.
October 6 2016 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala amezungumza na waandishi wa habari mkoani hapo na kuelezea mazingira halisi ya tukio hilo..
‘Tukio lilitokea Sept 26 mwalimu Frank Msigwa alitoa jaribio kwa wanafunzi lakini baadhi ya wanafunzi hawakufanya, wanafunzi walipewa adhabu ya viboko lakini Sebastian akakataa kuchapwa ndipo walimu wakamchangia kumpiga na kutoroka‘ –Amos Makala
‘Licha kwamba watuhumiwa wametoroka tangu siku ya tukio lakini nimeagiza vyombo vya sheria kuwasaka popote pale walipo, hadi sasa walimu wote wa shule hiyo akiwemo mwalimu mkuu wanashikiliwa ktk kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa maelezo‘ –Amos Makala
No comments:
Post a Comment