MOURINHO : BAHATI HAIKUWA YETU, TUNGESTAILI KUSHINDA KWA MABAO 7 AU 8 DHIDI YA STOKE
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa wangefaa kushinda na zaidi ya mabao 7-0 dhidi ya Stoke.
Mourinho ambaye anmeonekana kutoamini matokeo ya 1-1 baada ya kutawala mechi yote, anasema kuwa mchezo wa timu yake uliimarika zaidi ya mechi zote walizocheza msimu huu.
''Mchezo wetu ulikuwa wa kiwango cha hali ya juu sana.tulibuni fursa nyingi za wazi kabla ya kipindi cha kwanza na hata baada ya kipindi cha kwanza.tulifaa kuwa juu kwa zaidi ya mabao saba ama hata nane'', alisema baada ya mechi hiyo
Anasema kwamba licha ya fursa za magoli kuwa wazi bahati haikuwa yao.
No comments:
Post a Comment