REKODI 3 ZILIZOWEKWA BAADA YA MAN UTD KUPOKEA KIPIGO CHA 4 - 0 KUTOKA CHELSEA

united-02

Jose Mourinho amedhalilishwa aliporejea kwenye klabu yake ya zamani Chelsea akiwa na kikosi cha Manchester United kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
The Blues ambao walimtimu Mourinho kwa mara ya pili msimu uliopita, walipata goli la kuongoza baada ya sekunde 30 za kipindi cha kwanza baada ya Pedro kupachika mpira kambani kufatia makosa ya safu ya ulinzi ya Manchester United.
Gary Cahill akafunga bao la pili dakika ya 21 baada ya safu ya ulinzi ya United kuruhusu mpira wa kona uliopigwa na Eden Hazard kundunda kwenye eneo la penati box.
United walijaribu kutafuta angalau goli litakalowarudisha mchezoni, lakini hawakufanikiwa katika hilo na kujikuta wakishindwa kumdhibiti Hard ambaye alifunga akiwa umbali wa takribani mita 15 kutoka golini.
united-01
N’Golo Kante akawatoka mabeki kwa style ya aina yake na kupachilka bao la nne lililoihakikishia timu yake ushindi uliowafanya wawasogelee vinara wa ligi hiyo Manchester City kwa tofauti ya pointi moja.
United wanashika nafasi ya saba na gap kati yao na vinara wa ligi linaongezeka na kuwa pointi sita ikiwa karibia robo ya msimu imeshakatika.
  • Ilikuwa ni kipigo kikubwa kwa Jose Mourinho kwenye mashindano yote tangu alipokuwa Real Madrid alipochezea kichapo cha goli 5-0 kutoka kwa Barcelona November 2010.
  • Manchester United wamechezea kipigo kikubwa kwenye Premier League tangu walipofungwa 6-1 na Manchester City October 2011.
  • Ni kipigo kikubwa kwa United kwenye mechi za ugenini ndani ya Premier League tangu 1999 walipopoteza pia dhidi ya Chelsea.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.