YANGA YAIGOMEA BARUA YA KUJIUZULU KWA HANS VAN PLUIJM , WAZIRI NCHEMBA ASAIDIA KUMUOMBA ABAKIE KUINOA YANGA
Zikiwa zimepita siku nne tangu kocha mkuu wa Yanga Hans van Pluijm kuamua kuuandikia barua ya kujiuzulu kuifundisha klabu ya Yanga, uongozi wa klabu hiyo leo umemuandikia barua kumuomba Hans abadili maamuzi yake na kurejea kwenye benchi la ufundi kuendelea na majuku yake kama kawaida.
Kwa mujibu wa habari za ndani ya Yanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba alikutana na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deudetit pamoja na Hans van der Pluijm na kumshawishi kocha huyo raia wa Uholanzi kuachana na uamuzi aliuchukua awali.
Mh. Nchemba ambaye ni shabiki mkubwa wa Yanga amekuwa karibu na klabu hiyo tangu Hans alipotangaza kujiuzulu nafasi yake. Siku moja kabla ya mchezo kati ya Yanga na JKT Ruvu, Mh. Nchemba aliwatembelea wachezaji kambini na kuzungumza nao ikiwa kuwatia moyo kutokana na kuondokewa na kocha wao.
No comments:
Post a Comment