FRIDAY | XO : SIRI USIYOIJUA ILI KUFURAHIA MAHUSIANO YAKO

Image result for happy  AFRICAN couples images

Tabasamu lako ndiyo ishara kwamba upo tayari kwa ajili ya somo linaloendelea hapa katika FRIDAY XO  Marafiki zangu, kukunja uso ni tatizo, furaha ni tiba. 

Tafuta kufurahi mara nyingi kadiri uwezavyo ili kukuongezea siku zako kuishi hapa duniani, Ndivyo wataalam wanavyosema, tabasamu lako linakuongezea muda zaidi wa kuendelea kuwa chini ya uso wa dunia, huzuni ni ishara ya kupunguza umri wa uhai wako. 

Katika FRIDAY XO, leo mada inahusu siri za kufurahia mapenzi, sasa twende sawa kama ifuatavyo...

Kuna baadhi ya marafiki wana fikra potofu (hasa wanaume),Hawa wanaamini kumpa mwanamke nafasi katika maisha ni kumfanya akukalie. Si kweli, Mwanamke unapompa nafasi ya kwanza, anaufurahia uhusiano wenu, Anajiona mwenye hadhi kubwa zaidi kwako.

Hutafuta njia za kukufanya umpende maradufu, kuliko kumuacha akijiona hana nafasi, Ongozana na mpenzi wako kwenye kumbi za burudani, mialiko ya sherehe mbalimbali, lakini pia mpe kipaumbele kwa kila kitu.

Hili halihitaji elimu ya darasani, chunguza wenzako wanaowapa wenzi wao kipaumbele wanavyoishi, achana na mifumo ya kizamani, ukimpa mwenzako usawa anajiona hana nafasi kwako na thamani katika uhusiano mlionao.



Hakuna kitu kikubwa sana, ni kiasi cha kumpa nafasi katika mambo yako muhimu, Mathalani unataka kununua kiwanja, Hata kama umeshaweka kila kitu sawa, lakini kumshirikisha tu, kutamfanya ajione mwenye nafasi kubwa kwako.

Hili si kwa wanaume pekee, hata wanawake nao wanapaswa kutoa vipaumbele kwa wanaume zao
Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuongeza ladha ya mapenzi kwa wapendanao, Inawezekana elimu hii imekupitia kushoto, hebu jaribu uone mafanikio yake,kumpa nafasi mwenzako katika mambo yako, tafsiri yake ni kumuamini na kumfanya azidi kujiamini kwako.

Ni rahisi sana, lakini habari njema kwako ni kwamba, atakusikiliza kwa kila kitu, maana anajiona yeye ni sehemu yako kikamilifu

Mapenzi ya siri yana ukomo wake marafiki zangu. Ngoja niwaambie, unapokuwa unapenda mapenzi ya siri sana, unampa wakati mgumu mwenzako. 

Ni rahisi kufikiria kwamba, unafanya hivyo kwa kuwa ama hujiamini au una mtu mwingine. Weka mambo hadharani. Mtambulishe mwenzi wako kwa marafiki zako, Jiamini, unapokutana na mtu uliyesoma naye zamani au kuishi naye sehemu moja, mwambie kwamba uliyenaye ni mwenzako na unatarajia kuingia naye kwenye ndoa.

Kufichaficha kunaondoa utamu wa mapenzi. Kunazidisha maswali ambayo hayana majibu. Kama yapo ni huyo mwenzako kujijibu mwenyewe. 

Kwa kawaida, hatajipa majibu mazuri.  Yatakuwa ya kinyume – yenye tafsiri mbaya. Kwamba yawezekana hutaki kumtambulisha kwa kuwa una mtu mwingine. Je, ni kweli? Kama ndivyo huna sababu ya kumpotezea muda mwenzako. Kama si kweli, basi amka. Gundua kwamba ulikuwa unafanya makosa na uanze ukurasa mpya.


Nakutakia Ijumaa njema na yenye baraka.

FRIDAY XO 

LETS TALK BOU LOVE.~

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.