SIR ELTON JOHN AMEKATAA KUTUIMBA KATIKA HAFLA YA KUAPISHWA KWA DONALD TRUMP

Mwanamuziki Sir Elton John

Mwanamuziki Sir Elton John hatowatumbuiza wageni katika sherehe ya kuapishwa kwa Donald Trump, msemaji wa msanii huyo maarufu amesema.
Anthony Scaramucci,mmoja wa kikosi cha mageuzi cha bw Trump,aliambia kipindi cha televisheni cha BBC HARDtalk kwamba Sir Elton atawatumbuiza mashabiki mjini Washington DC mwezi Januari.
''Elton ataandaa tamasha wakati wa sherehe za kuapishwa kwa bwTrump'', Scaramucci amesema
Lakini jambo hilo lilipingwa na mwakilishi wa Sir Elton mjini London.
''Hakuna ukweli wowote kuhusu swala hilo,'' aliambia BBC
Wakati wa kampeni ,Sir Elton alikuwa akionyesha dalili za kumuunga mkono mpizani wa bw Trump,bi Hillary Clinton wa chama cha Republican.
Akiwatumbuiza mashabiki katika hafla ya uchangishaji wa pesa, ya bi Clinton mjini Los Angeles mwezi Oktoba, aliripotiwa kuuambia umati kwamba: ''Tunahitaji mtu mwenye ubinadamu katika ikulu ya White House,na siyo mtu mjinga''
Bw Trump alikuwa ametumia wimbo wa Sir Elton Rocket Man and Tiny Dance bila idhini ya mwanamuziki huyo katika kampeni zake.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.