2016 UMEKUWA MWAKA WA SINGELI KUKUA,HIZI HAPA TAKWIMU ZA MUZIKI HUO NA MATARAJIO YA 2017
Mwaka huu Singeli imezalisha majina makubwa ya wasanii kama Man Fongo, Sholo Mwamba na wengine.
Muziki huo uliokuwa maarufu kwenye sherehe za uswahilini na vichochoroni jijini Dar es Salaam na kutafsiriwa kama wa wahuni na wavuta bangi, umefanikiwa kuingia mainstream na redio kuzicheza kama nyimbo zingine.
Mwaka 2016, kituo cha redio cha EFM, kitakumbukwa kwa mchango kwenye kusaidia kueleweka kwa muziki huu kupitia jitihada zake za kuucheza kwa wingi.
Baada ya muda redio zingine nazo zikaanza kucheza baadhi ya nyimbo za wasanii wa Singeli ambao walianza kupata nafasi za kutumbuiza kwenye majukwaa ya kawaida na kulipwa fedha kama walipwavyo wasanii wa Bongo Flava.
Lakini pia nguvu ya muziki wa Singeli uliweza kuwavutia wana hip hop wakiwemo Profesa Jay, Roma na Baghdad pamoja na msanii wa R&B, Rama Dee kuweka vionjo vyake kwenye nyimbo zao.
“Nimefanya hip hop singeli kwaajili ya kuupeleka muziki huo mbali lakini pia kuitengeneza hip hop tofauti,” alisema Profesa.
“Kuliko kuwakopi akina Lil Wayne wanafanyaje basi tufanye muziki ambao tutakopi muziki wa nyumbani. Nadhani ni muda sasa hivi wasanii wa hip hop kutanua, wasikopi vya Marekani, wako vya Tanzania ili kuifanya hip hop yetu ibadilike kila siku,” aliongeza.
Na hata Vanessa Mdee alisema Singeli ni muziki wa aina yake.
Vanessa pia anautabiria makubwa muziki huo. “The drum percussion is so unique,” alikiambia kipindi cha 5 Select cha EATV miezi kadhaa iliyopita.
Vanessa pia anautabiria makubwa muziki huo. “The drum percussion is so unique,” alikiambia kipindi cha 5 Select cha EATV miezi kadhaa iliyopita.
Vee Money aliongeza kuwa maproducer wakubwa kama Major Lazer na Pharrell Williams wamekuwa wakiufuatilia muziki wa Afrika kwa ukaribu na huenda masikio yao yakaja kutua kwenye muziki wa Singeli.
Belle 9 na Juma Nature kwa upande wao walikuwa na mtazamo tofauti.
“Sitegemei kufanya Singeli,” alisema Belle. “Hata kama nitafanya, sitofanya kama release song sababu Singeli ni muziki fulani hivi ambao unapita, ni bubble gum music. Sasa hivi watu wanaushabikia lakini itafika time utapita, sio muziki wa kustick.”
Naye Nature alisema, “”Singeli itapita tu kwasababu ya uhuni,” ; “Unajua raia wengi wa Bongo hawapendi mambo ya kipumb*vu pumb*vu na mashabiki wetu wengi sana sio wahuni ila wahuni wanakuja katika hizi section, so wakija kwenye section hapo muziki hakuna tena,”
Swali ni je? Muziki huo utaendelea kufanya vizuri mwaka 2017?
No comments:
Post a Comment