Naomba nikuulize wewe mwenzangu ambaye upo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye unahisi ndiye sahihi kwako, ghafla unaingiwa na hisia ambazo katika mapenzi zinakuwa zinauweka uhusiano wako rehani, Je unazifahamu hisia ambazo ni hatarishi kwako ?? Ungana nami...
>>> NASALITIWAKuishi katika mapenzi huku ukiwa na fikra kwamba mwenza wako anakusaliti ni jambo baya kwa vile huathiri msukumo wa ndani wa kupenda. Matokeo yake utajikuta ukishindwa kutimiza wajibu wako ama mke/mume kwa sababu tu ya kuendekeza hisia mbaya, acha kuhisit afuta ukweli.
>>> TUTAACHANAKuna wapenzi ambao wanaishi na mawazo ya “ipo siku tutaachana”, Wanafanya hivyo eti kwa kutafsiri mwenendo usio ridhisha wa mapenzi yao, Kusema kweli hili ni jambo baya kwani huondoa ari na kujenga ufa wa mapenzi.
Huwafanya wapenzi kubakia na wazo moja tu, la kutafuta sehemu mbadala ya kwenda baada ya kuachana. Usiwaze kabisa kuachana hata kama mnagombana na mwenzako kila siku.
>>> SIWEZI MAPENZIBaadhi ya wapenzi huwa na hisia kwamba hawayawezi mapenzi,Hata kama hawaja ambiwa chochote kuhusu kuto watosheleza wenza wao faragha hivyo hukimbilia kujihukumu wenyewe wakati hujaambiwa kama echeza chini ya kiwango, hofu ya nini? Usiwaze hivyo, kama na lolote linalo kufanya uwe na hofu muulize mwenzio.
>>> NINA KASORO
Naamini mitaani wapo watu ambao huamini wana kasoro fulani ndiyo maana hawafikii viwango vya kupendwa kama wanavyohitaji, “Yaani mimi ningekuwa kama fulani ningefurahi sana lakini ufupi wangu ndiyo tatizo.” Hizi ni hisia mbaya tu, kumbuka kuna wafupi wanapendwa ile mbaya, Jisahihishe na epuka kujishusha hadhi kwenye hisia zako.
>>> NIMEKOSEA KUCHAGUAUsijihukumu makosa kwa sababu umeona mpenzi wako ana tatizo fulani. Fahamu kuwa kasoro ni sehemu ya ubinadamu. Weka mikakati ya kumuongoza mwezio kuliko kuhitimisha kwa mawazo kwamba ulikosea kumchagua. “Ningejua kama yuko hivi nisingemchagua.” Usiwaze hivi!
>>> UNANIDANGANYA
Ipo aina ya watu ambao hata kama wakiambiwa wanapendwa sana, hukimbilia kusema na kuamini kuwa wanadanganywa. “Mmm unanidanganya.” Atasema hivyo licha ya kuona mwanaume anavyojituma kumsotea na kumuonesha kila dalili za mapenzi. Hili ni jambo baya, ukithibitisha kwamba unapendwa usihisi unadanganywa, utapoteza bahati yako.
No comments:
Post a Comment