HII NI GOOD NEWS KWA WAPENZI WA " DA WEEKEND CHAT SHOW " KUTOKA SHILAWADU

img_7516

The Weekend Chat Show ni moja ya vipindi pendwa vya TV kwasasa kutokana na maudhui yake ya kufichua Umbea au Ubuyu kama wao wanavyoita, ubuyu ambao unawahusu mastaa mbalimbali.

Ubuyu huo umezaa jina kubwa hapa nchini la Shirika la Wambea Duniani yaani SHILAWADU jina ambalo kila mtu analifahamu kwa umahiri mkubwa kabisa wa watangazaji wa kipindi hicho kutoka Clouds TV Soudy Brown na Qwhisar Thomson wanakuletea Shilawadu Ubuyu Tour itakayo anza siku ya leo Desemba 24 kwa wakazi wa wilaya ya Temeke, Tour hiyo ni ya nchi nzima, kwa lengo la kuwashukuru watazamaji wao kwa kuwafanya kuwa kipindi kinachotazamwa zaidi, pia watazamaji hao watakutanishwa na mastaa mbalimbali na kuwatolea mapovu live.


Akizungumza Jijini Dar es Salaam mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho Qwhisar Thomson amesema kutakuwa na Gari maalum kwaajili ya watazamaji wa kipindi hicho na wataingia kwa kununua tiketi zinazopatikana katika ofisi za Clouds Media Group kwa shilingi 15000 na Tour hiyo itafanyika kila siku za Weekend, na kuongezakuwa wameamua kutumia fursa kwa kuwa wajasiriamali wa kuuza Ubuyu ili kujiongezea kipato.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.