KUTANA NA MHUBIRI WA KIISLAMU ALIYEKUA NA WAKE 86 NA WATOTO 203

Mohammed Bello Abubakar huenda alikuwa na zaidi ya wake 1

Mhubiri mmoja wa zamani wa Kiislamu nchini Nigeria ambaye alikuwa na takriban wanawake 86 ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 93.
Mohammed Bello Abubakar alifariki nyumbani kwake katika jimbo la Niger siku ya Jumamosi, kutokana na ugonjwa ambao haukutajwa
Watu wengi walihudhuria mazishi yake siku ya Jumapili.
Gazeti la Nigeria la Daily Trust liliripoti kuwa alipokuwa na wake 86 mwaka 2008 wakati aliangaziwa na vyombo vya habari, idadi hiyo ilipanda hadi wake 130 wakati wa kifo chake.
Wengine wao walikuwa wajawazito.
Mwaka 2008 alikuwa na takriban watoto 170 lakini amewaacha watoto 203

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.