IMENIFIKIA LIST MPYA YA RC MAKONDA WATUHUMIWA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA..VANESSA MDEE,TUNDA NDANI


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemkabidhi Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro majina mapya ya watu wanaotuhumiwa kuhusika kwenye mtandao wa biashara ya Madawa ya kulevya.

Na katika kuhakikisha haupitwi mtu wangu, nimeinyaka list hiyo na nimekuekea hapa,, 


RC Makonda amesema wale walioitwa leo kituoni hapo bado wanaendelea kufanya nao mahojiano na kama kuna yeyote atakayekutwa na hatia sheria itachukua mkondo wake.
Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa hii, RC Makonda aliliagiza jeshi la polisi kuwakama wale ambao hawajaripoti leo kama walivyoagizwa jana huku akiwataka wale waliotajwa leo kuwasili Kituo Kikuu cha Polisi Dar es salaam Jumatatu.
“Upande wa askari majina mapya ni 
Mudy Zungu, 
Fadhili na 
Beny, 
nikisema hivyo askari wanajua jinsi ya kuwapata, hawa watatu waunganishe kwenye ile list ya nyingine waandelee kushughulikiwa. Mali zao zipo na mwingine amenunua nyumba Kigamboni kupitia pesa na Madawa ya kulevya,” alisema Makonda.
 “Lakini kwa upande wa ndugu zangu ambao Jumatatu wanatakiwa kuwepo hapa, na ningeomba sana waandishi wa habari munisaidie, musizifanye stori zenu zikaonekana ni madawa ya kulevya na wasanii, ni Madawa ya kulevya kwa sababu nimeona baadhi ya watu wanaifanya ni mali ya wasanii, kwa hiyo ni kila sehemu tunagusa kama hao watu wapo. 
Kwa mfano:  kuna mtu mmoja anaitwa Omary Sanga, huyu ni mmoja kati ya watu waliosababisha sio chini ya watu 70% waliofungwa China kwajili yake, ni yeye alikuwa anawapeleka, sasa hivi yupo Dubai ana process za kwenda China lakini tutamkamata. 
Kuna mwingine anaitwa Kashozi, mwingine anaitwa Amani, kuna mwingine anaitwa Alidali Kavila, kuna mwingine anaitwa Tunda pamoja na dada yangu Vanessa Mdee,”

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.