MOURINHO KIKAANGONI FA - MATAMSHI YAKE JUU YA MWAMUZI WA MECHI YA LEO DHIDI YA LIVERPOOL

Image result for mourinho
Matamshi ya Jose Mourinho kuhusu uteuzi wa mwamuzi anaeshabikia Manchester United Anthony Taylor kwa mchezo wa ligi kuu England kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool utakaochezwa leo jumatatu yatachunguzwa na Shirikisho la Mpira wa miguu nchini humo FA.
" Mourinho amesema itakuwa vigumu kwa mwamuzi huyo kuchezesha vizuri baada ya uteuzi wake kukosolewa."
'Mtu mmoja akiwa na lengo anaweka shinikizo kwake' alisema Mourinho
Kwa kawaida makocha hawatakiwi kuzungumza lolote kuhusiana na mwamuzi kabla ya mchezo.
Anthony Taylor hajatoa kadi yoyote nyekundu msimu huu
FA inataka kuchunguza matamshi hayo kabla ya kuamua ni hatua gani kama ipo inaweza kuchukuliwa.
Uteuzi wa Taylor, umekosolewa na Kenith Hackett,mkuu wa Bodi ya marefarii Professional Game Match Officials Ltd

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.