" MUZIKI BILA MADAWA INAWEZEKANA " MANENO YA T. I.D BAADA YA KUONANA NA MAKONDA LEO




Msanii wa kizazi kipya nchini TID ambaye siku kadhaa zilizopita amehusishwa na matumizi
ya madawa ya kulevya, amefunguka na kusema muziki bila madawa ya kulevya inawezekana.
TID ambaye leo amekutana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda 
Anasema kuwa amepata nafasi ya kukaa na kujadili na kiongozi huyo kuona namna gani
wanaweza kuoka vipaji vya wasanii.
"Muziki bila madawa ya kulevya inawezekana..This is the turning Point kwangu mimi
na kizazi cha muziki huu wa kizazi kipya, nikiwa na Mhe. Makonda leo tukijadili 
jinsi gani ya kuokoa Vipaji na sanaa kwa ujumla, Mungu ibariki bongo fleva, 
Mungu ibariki Tanzania" aliandika TID 
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda alikuwa na haya
ya kusema baada ya TID kumtembelea leo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. 
"Mungu wetu hajalala na siku zote anampenda amtafutae, karibu tea nyumbani T I D" 
aliandika Paul Makonda. 

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.