SHINDANO LA DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE KUANZA RASMI APRIL MOSI


Mashindano ya Dar es salaam Stock Exchange Scholar Investment Challenge, yamefunguliwa leo rasmi, kwenye mkutano ulifanyikia katika ofisi za soko hilo la hisa lililoko jijini Dar es salaam, Ohio street, ikihudhuriwa na Waliokuwa washindi kwenye top 10 mwaka uliopita kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha. 

Katika hafla hiyo, chuo cha uhasibu arusha, kilipewa nafasi ya kuwa wenyeji katika ufunguzi huo kutokana na ushiriki wao katika mashindano hayo, ambapo kilitoa mshindi wa shindano hilo msimu uliopita. 

Akizungumza aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla, Dr. Faraj Kassid, kaimu mkuu wa chuo cha Uhasibu Arusha, amewahasa wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nhini kushiriki katika mchezo huo utakao jenga uelewa wao katika maswala ya hisa nchini na jinsi unavyofanya kazi.

Dr. Kassid aliongeza, " kutafuta elimu kuna namna tofauti, tofauti, unaweza kupata elimu ukiwa darasani ukiwa na mwalimu wako au ukapata elimu ile kwa wewe mwenyewe kujifunza, DSE wametuletea platform ya wanafunzi wenyewe kujifunza kwa vitendo. "

DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE ni shindano ambalo limeandaliwa kwa ajili ya Wanafunzi wote wa Vyuo vya Elimu ya Juu na Shule za Sekondari Nchi Nzima
Shindano hili linaratibiwa na kuendeshwa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kila mwaka kuanzia tarehe 1 Aprili hadi tarehe 30 Juni.
 
Shindano la DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE 2017 limedhaminiwa na CRDB Bank; SWISSPORT Tanzania; na FSDT. Vile vile mfumo wa ushiriki katika hili shindano kwa njia za simu na internet umewezeshwa na Mitikaz Limited na Maxcom Africa.
 
Kwa mara ya Kwanza Shindano la mwaka huu litashirikisha Wanafunzi wa Shule za Sekondari katika Shindano Maalum la Uwekezaji kwa kupitia mfumo wa kiTeknohama unaofikiwa kwa njia ya tovuti ya www.younginvestors.co.tz.
 
Wanafunzi wanaweza kushiriki kwenye hili shindano BURE:
  1. Kupitia tovuti ya www.younginvestors.co.tz
  2. Kupitia Application ya Smartphone ya Leverage Scholar
  3. Kupiga namba ya simu ya *150*36#  

Lengo la DSE la kuelimisha Wanafunzi linapakana na Lengo la Shirika la kimataifa la Child & Youth Finance International. Shirika hili la kimataifa limetenga wiki hii iliyoanza tarehe 27 Machi na kuisha leo hii tarehe 31 Machi kuwa Wiki Rasmi ya Fedha Duniani au Global Money Week kwa mwaka 2017.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.