55th OBAMA BIRTHDAY, KENDRICK LAMAR, JAY & B KUTUMBUIZA.


obama

Obama atasherehekea kufikisha miaka 55 usiku wa Ijumaa hii kwenye ikulu ya White House na kuhudhuriwa na mastaa kibao.
Mtandao wa Page Six umeripoti kuwa Michelle Obama anaangusha party ya siri ya kukata na shoka kwa Obama kusherehekea birthday yake ya mwisho akiwa kama rais.
Umedai kuwa Usher atatumbuiza kwenye sherehe hizo pamoja na Kendrick Lamar ambaye Obama anamkubali sana. Wageni wengine ni pamoja na Ellen DeGeneres, Sarah Jessica Parker, Stevie Wonder, Jennifer Hudson, John Legend na Magic Johnson.
Wanasiasa watakaokuwepo ni pamoja na mgombea urais mwaka huu wa chama cha Democratic, Hillary Clinton na makamu wa rais, Joe Biden.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.