HII KALII.. MSANII WA KIUME UFARANSA ATAMIA MAYAI YA KUKU KWA SIKU 21 - 26

Abraham Poincheval Paris, Ufaransa Machi 29, 2017.

Msanii kutoka Ufaransa Abraham Poincheval anaendelea kutamia mayai ya kuku akiwa na matumaini kwamba mwishowe yataangua vifaranga.
Msanii huyo anatumia joto kutoka kwa mwili wake kutamia mayai hayo 10.
Poincheval ambaye hufanya uigizaji wa kuigiza mambo ya ucheshi lakini ya hatari tayari ameishi wiki mbili ndani ya dubu, miongoni mwa mambo mengine ya kushangaza.
Atakuwa katika chumba maalum ambacho anatamia mayai, ambapo watalii wanaweza kumtazama katka makumbusho ya Palais de Tokyo mjini Paris.
Anatarajia kutamia mayai hayo kwa siku 21 hadi 26.
"Kusema mweli, kimsingi, ni kama nimekuwa kuku," anasema
Poincheval, 44, ameuita uigizaji huo wake - "Oeuf" (Yai kwa Kifaransa).
Badala ya kutamia mayai hayo kwa kuchutuma juu yake moja kwa moja, anatumia kiti maalum ambacho kina mfuko eneo lake la kukalia. Hapo ndipo mayai hayo yamewekwa.
Poincheval atakuwa amejifunga blanketi kuzuia joto kupotea.
Aidha, anapanga kula vyakula vinavyoongeza sana joto mwiliki, kama vile tangawizi.
Wakati wa haja, atatumia kijisanduku kidogo kilichomo mvunguni mwa kiti chake.
Ndipo mayai hayo yaangue vifaranga, hahitaji kuondoka zaidi ya dakika 30 kwa siku. Anapanga kutumia muda huo kula chakula.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.