WENGER AWAPA SIFA MASHABIKI WA ARSENAL, JAPO WALIANDAMANA KUMPINGA

Image result for arsene wenger

Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema mashabiki wa klabu hiyo walikuwa wazuri sana wakati wa mechi dhidi ya Manchester City ambayo iliisha kwa sare ya 2-2 uwanjani Emirates.

Amesema hayo licha ya kwamba bado wapo mashabiki walioandamana kumpinga wakati wa mechi hiyo ya Jumapili.
Wenger, ambaye anakabiliwa na shinikisho baada ya kushindwa mechi moja pekee kati ya sita walizocheza karibuni amekuwa akitakiwa na baadhi ya mashabiki ajiuzulu.
“Lazima niseme kwamba, licha ya yote yaliyofanywa na baadhi ya mashabiki, mashabiki wetu walikuwa wazuri sana jana,” alisema Mfaransa huyo baada ya mechi.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.