TERRY PECK, MSANII ALIYEJITUPA BAHARINI ILI KUKWEPA KULIPA BILL YA CHAKULA

Mwanamuziki ajitosa baharini kukwepa kulipa bili ya chakula

Mwanamume mmoja raia wa Australia ambaye alikuwa na bili kubwa ya kulipa baada ya kupata mlo kwenye mgahawa mmoja aliruka na kuingia baharini ili kukwepa kulipa bili hiyo.
Polisi walimfuata kwa kasi mwanamuziki hiyo ambaya baadaye alisema kuwa alikimbia kumsaidia rafiki yake kujifungua mtoto katika fukwe za bahari.
Alikuwa na bili ya zaidi ya dola 450.

Terry Peck ambaye amefunguliwa mashtaka ya wizi baadaye alidai kuwa chakula hicho hakikua kimepikwa kwa njia inayotakikana.
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 33 alifikishwa mahakani baada ya kisa hicho kilichotokea katika mgahawa wa Omeros Bros.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.