DIAMOND, RICH MAVOKO WATAJWA KUWA WASHIRIKINA
Kumekuwepo
na story nyingi juu ya kuwepo kwa ushirikina kwa baadhi ya wasanii iwe
wa bongo movie au bongo fleva,wao wamekua wakiutaja sana pasipo kutaja
majina ya hao wanaojihusisha na ushirikina huo.
Lakini
moja kati ya wadau wa muziki na aliyewahi kuwa meneja wa baadhi ya
wasanii,pasipo kupepesa maneno ametaja baadhi ya wasanii ambao anakiri
kuwahi kuwapeleka kwa waganga wakienyeji ili wakafanye ushirikina.
Diamond
platinumz,rich mavoko na sam wa ukweli,wametajwa na maneno kama wasanii
aliowahi kuwapeleka kwa waganga kwa ajili ya kufanya dawa,akizungumza
na kipindi cha planet bongo cha East Africa radio maneno ametabainisha
hayo.
“Ndele
ni sehemu ambayo baadhi ya wasanii waliiamini sana lakini Mungu akisema
‘Yes’ ni ‘Yes’ tu kwa hiyo nakumbuka wasanii ambao nilikwenda nao kwa
waganga kuroga ni pamoja na Rich Mavoko tena tulienda mbali kabisa huko
Kigamboni ndani ndani huko tumeenda ndugu yangu, nilisharusha nazi
katikati yaani usiku ule unajifanya chizi kama umevurugwa,” Meneja
Maneno alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Lakini
anamtaja diamond kama ndo kinara wa wa mambo hayoAliongeza, “Hata Sam
wa Ukweli siwezi kukataa, ni watu ambao imani yao iliwapeleka huko
lakini mimi nakumbuka kazi yangu niliyokuwa nafanya sikutaka kwenda kwa
waganga…. ila sasa huyu Mondi sasa nimepata taabu naye, mara leo twende
kwa mjomba, tunapeleka unga, leo tunapeleka mchele na mganga alivyo
mshenzi hajawahi kuagiza samaki, yeye ni jogoo, mbuzi,”
No comments:
Post a Comment