TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA
Hiki
ni kipindi ambacho ligi na mashindano mengi yamemalizika,huku machache
yakimaliziwa mwezi huu kukamilika tayari vilabu mbalimbali vimeanza
kusajili wachezaji kwa ajili ya kujiandaa kwa msimu ujao wa ligi.
Nchini
england klabu ya westham imekamilisha usajili wa aliyekua beki wa
Manchester city pablo zabaleta kwa uhamisho huru kufuatia kumaliza
mkataba wake baada ya kuitumikia klabu hiyo ya jiji la Manchester kwa
takribani miaka sita.
Kwingineko
manchester city wanaonekana kua kwenye nafasi nzuri ya kumsajili
mchezaji wa klabu ya monaco na timu ya Taifa ya ureno benardo
silva,kiungo huyo mwenye umri wa miaka,22 alikua akifuatiliwa kwa karibu
na klabu ya Manchester United,lakini city wanaonekana kua kwenye nafasi
kubwa zaidi.
Naye
nahodha wa Manchester United, mshambuliaji wayne rooney anatajwa
kukaribia kutoa mkono wa kwa heri kwa klabu ya Manchester United,huku
akitajwa kuelekea nchini china,rooney ambaye nafasi yake katika kikosi
cha manu imekua shakani hali iliyopelekea kuachwa katika kikosi cha timu
ya taifa.
No comments:
Post a Comment