Mastaa watakaoperform BET Awards 2017 imetoka, mmoja anatoka Afrika
Sherehe ya utoaji wa Tuzo maarufu za muziki duniani BET inatarajiwa kufanyika June 25, 2017 kwenye Ukumbi wa Microsoft Theaterkatika Mji wa Los Angels, Marekani huku kukitarajiwa pia kuwa na show kubwa kutoka kwa mastaa mbalimbali duniani.
June 1, 2017 imenifika list ya mastaa watakaofanya performance siku hiyo ambapo mpaka sasa msanii aliyetajwa kwenye list hiyo kutoka Africa ni ‘Starboy’ Wizkid waNigeria ambaye atapanda stage moja na mastaa kama Kundi la Migos, Kendrik Lamar, Tamar Braxton, Wiz Khalifa, Pusha T,Desiigner, Bryson Tiller, Rae Sremmurd,Jhené Aiko, New Edition na wengine kibao.
Licha ya kutajwa kwenye list hiyo Wizkid pia anawania tuzo ya Best African Act 2017kwenye tuzo hizo za BET huku miongoni mwa wasanii ambao watakuwepo katika sherehe hizo ni pamoja na Mtanzania RayVannyambaye ametajwa kuwania tuzo ya Viewers Choice Awards 2017.
No comments:
Post a Comment