TID - " ACHA QUICK ROCA ANUNUE LAMBORGHINI "



Quick Rocka na kundi la OMG waliachia siku chache video ya wimbo " Watasema " huku TID akidai wametumia melody na maneno ya wimbo wake bila ridhaa yake hivyo kutaka alipwe fidia ya Tsh. 20m.
June 27, 2017 kwenye XXL ya Clouds FM ikiwa ni Eid Pili ambapo wamekutana TID  na Quick Rocka pamoja na OMG, TID akiulizwa kama ni yeye ndiye aliyepost na kwa nini alichukua uamuzi wa kudai fidia na majibu yake yalikuwa hivi:
”Ukweli ni kwamba hawa jamaa walitakiwa wanilipe lakini tumekubaliana. Wamekuja tumepozana ili mwisho wa siku kuendeleza muziki mzuri. Nilipanic nikasema Rocka ndio anatoboa sasa hivi nitamuona na Lamborghini.
“Halafu huu wimbo umechukua tuzo mbili, kama East Africa Best Collaboration Song na Best Video kwa kipindi kile. Ulikuwa wimbo mkali sana halafu ulinicost hela nyingi. Nilirecord Kenya, Home Boys walinicharge kama 1.5m za kitanzania kufanya kila kitu lakini mwisho wa siku nimeona kafanya kitu kizuri.
“Pesa siyo kitu sana kama ameweza kufanya A, B, C, D kwa lengo la muziki mzuri nimempa blessing zangu acha anunue Lamborghini.” – TID. 

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.