LOWASSA AHOJIWA MASAA NNE, ACHIWA KWA DHAMANA...HII HAPA SABABU YA KUITWA NA DCI
Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Edward Lowassa ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa saa manne katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) leo jijini Dar es salaam.
Kibatala ambaye ni mwanasheria wa CHADEMA, amesema Lowassa amehojiwa kwa kosa la uchochezi na ameandika maelezo ya onyo juu ya kauli aliyoitoa wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.
“Mzee amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa Juni 23, mwaka huu wakati wa futari iliyoandaliwa na Waitara. Baada ya kuhojiwa ameandika Maelezo ya Onyo na atatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29,” amesema Kibatala.
No comments:
Post a Comment