Wenger akiri kumnyemelea mahrez

Arsene wenger akiri kumnyemela Ryad mahrez



Siku chache baada ya kuripotiwa kuwa ryad mahrez amewasilisha ombi rasmi la kuihama mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya England Leicester city,kocha wa klabu ya Arsenal arsene wenger amekiri kuvutiwa na mpango wa kumsajili mchezaji huyo.

Akihojiwa na chombo kimoja cha habari kocha huyo wa mabingwa wa FA,ambaye yupo kwenye presha kubwa kutoka kwa mashabiki  wa klabu hiyo juu ya kusajili wachezaji wakubwa  ametabainisha kutopeleka ofa rasmi kwa Leicester city.

‘Tumepeleka ofa ya kumtaka? Hapana bado,nikisema hapana bado namaanisha tunaweza kupeleka au kutopeleka’
Pamoja na Arsenal vilabu vya inter milan ya Italy na Monaco ya ufaransa vimetajwa kuvutiwa na mpango wa kumsajili nyota huyo wa Algeria mwenye umri wa miaka 26

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.