" NIKO SERIOUS NA SWALA LA NDOA " - SHILOLE
Wiki iliyopita watu walichukuliwa kama utani pale msanii wa Bongo Flava, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ aliposema ameshatolewa barua ya uchumba, lakini Shilole mwenyewe ameendelea kusisitiza kwa sasa yupo katika mahusiano serious na ndoa inafuata.
“Ni kweli nimechumbiwa panapo majaliwa yake Mwenyezi Mungu akijaalia nitafunga ndoa,” Shilole amesema hayo leo katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm.
Katika hatua nyingine Shilole amebainisha kuwa wimbo wake mpya ‘Kigori’ ameandikiwa na Barnaba na kuongeza ukimya wake ulitokana na kutaka kuwapa nafasi wasanii wapya wa kike kufanya kazi nzuri ila kwa sasa amerejea.
No comments:
Post a Comment