HATIMAYE SIR. ALEX FERGUSON ANENA....
EPL ya msimu ujao itakua na moja ya kocha bora kwenye ligi za Ulaya naye ni Pep Guardiola akiiongoza club ya Manchester City.
Sir Alex Ferguson mwenye miaka 74 ameulizwa swali kuhusu ujio wa Pep ndani ya EPL. “Bila kujiuliza maswali mengi Pep ana ethics nzuri kwenye kazi yake, anafanya hivyo kwenye muda wa mazoezi hadi muda wa mechi. Yeyote anayedhani kwamba Pep atashindwa kwenye EPL basi inabidi abadirishe mawazo. Man City wamefanya kitu kizuri kumchukua kwenye timu yao. Lakini Pep hata kutana na vitu virahisi kwenye EPL, kila kocha anayetoka nje ya England lazima atakwambia ugumu wa EPL. Pep anaweza kufanikiwa ndani ya EPL lakini sidhani kama atafikia level ya mafanikio kama alivyokua na Barcelona, ile ilikua level nzuri sana na walikua vizuri” hayo ndo majibu aliyotoa Mzee huyo mwenye heshima mjini Uingereza.
Pia, Sir Alex Ferguson ameongoea na Sky Sport kuhusu mbio za ubingwa msimu huu kwa jinsi ulivyo sasa hivi...
Kocha Ferguson ameshinda mataji 13 kwenye muda wa miaka 26 aliyokaa ndani ya Old Trafford, hivyo maneno yake kuhusu EPL lazima yachukuliwe serious.
Sir Ferguson anasema Tottenham Hotspurs ndio timu pekee yenye uwezo wa kuizuia Leicester City kwenye mbio za ubingwa. “Leicester wanakaribia kwenye mstari wa kumaliza kama mabingwa, hiyo ni task kubwa sana kwao. Wanatakiwa kuwa hivi hivi hadi mwisho na hawatakiwi kubadilika, wanatakiwa kuwa hivi hivi kama walivyokua kwa miezi 6 iliyopita”.
“Naiona Spurs pekee kuwa ni ya hatari kwa Leicester City. Spurs kwa sasa wanacheza soka zuri zaidi ya miaka mingi niliowajua kwa miaka kadhaa iliyopita. Leicester wamekua timu bora kwa msimu mzima na wanastahili kushinda ubingwa.” Alisema Sir.
No comments:
Post a Comment