BILLNAS MZEE WA " CHAFU POZI " ALAZIMIKA KUSIMAMISHA MUZIKI ILI AKAFANYE " SUPP " 3 ALIZOPATA
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Bill Nas amelazimika kusitisha kwa muda shughuli za muziki wake ili kuweka mambo sawa katika chuo anachosoma.
Rapper huyo ambaye anabukua katika chuo cha College of Business Education (CBE) jijini Dar es salaam amepata supplement tatu katika baadhi ya masomo yake.
“Bill Nas wiki anahitaji muda mwingi wa discussion kwa ajili ya supp zake, amepata supp tatu na baada ya wiki moja atarudi kwenye mishe za muziki,” alisema Mchafu. “Yaani hajapata maksi ambazo zilikuwa zinahitajika katika hayo masomo yake, anatakiwa kupata maksi zaidi ya 40, sasa amepata chini ya hapo kwa hiyo amelazimika kurudia mitihani,”
Chakoma amesema yeye kama meneja wa LFLG, atahakikisha Bill Nas anaendelea kufanya vizuri katika masomo na muziki.
“Mimi nimeanza kumsaidia Bill Nas hata kabla hajaanza muziki, kwa hiyo wakati anasoma ndo akaniambia broo nataka kufanya muziki, mimi nikamwambia kama unaweza poa, na wakati anaanza hatukuwa tunafanya muziki kama biashara kwa sababu tunajua kijana bado anasoma,”
No comments:
Post a Comment