UNAJUA NI NYIMBO ZA KINA NANI MH. RAIS MAGUFULI ANASIKILIZA?? NIMEKUSOGEZEA HAPA
Christian Bella na Mrisho Mpoto ni kati ya wasanii waliopo kwenye playlist ya Rais Dkt John Pombe Magufuli., Hadi sasa Rais ameonyesha kuwaelewa wanamuziki wawili wa bongo flavor lakini haimaanishi wengine hapendi kazi zao.
Akiongea kwenye kipindi cha Bongo Beatz cha Star TV, Bella alisema Rais Magufuli anamkubali hadi basi! Amesema kwake kukubalika na Rais wa nchi ni heshima kubwa na kumbukumbu atakayoitunza milele.
Bella amedai ni muhimu kwakuwa hajawahi kuwambia kitu kama hicho na rais yeyote tangu aanze kufanya muziki. “Ni kitu kikubwa sana kwangu na sikutegemea,” alisema.
“Sijawahi kuambiwa na na rais yeyote, rais wangu ni Magufuli nampenda sana,” alisema Bella.
Hivi karibuni Mrisho Mpoto naye alionesha furaha yake baada ya Dkt Magufuli kumwambia kuwa anaupenda wimbo wake ‘Sizonje.’
No comments:
Post a Comment