UCHAGUZI MAREKANI... Kipi kinaendelea uchaguzi wa marekani?

  AMERICA GENERAL ELECTION 


SATURDAY, MARCH 26, 2016

Donald Trump mtia nia mwenye damu ya kunguni






Licha ya kura za maoni zinazooenesha mgombea wa uraisi wa marekani kupitia repulican kuonesha anaongoza kwenye kura za maoni ndani ya chama chake, ni dhahiri kwamba viongozi wa chama hicho cha republican hawamtaki awe kama mgombea uraisi kupitia chama hicho.

Baada ya kugundua Trump aungwi mkono na viongozi wa chama hicho alitishia kuondoka na kwenda kusimama kam amgombea binafsi wa uraisi kitu ambacho kiliwapo kiwewe viongozi wa chama hicho cha Republican, pia alisisitiza kwamba atamuunga mkono mgombea yoyote atakaye chaguliwa na chama hicho  huku akisisitiza kwamba mgombe uyo atakua ni yeye(Trump) http://www.mwananchi.co.tz/Donald-Trump-mtia-nia-mwenye-damu-ya-kunguni/-/1596774/3134398/-/sct49q/-/index.html

Miongoni mwa vigogo waliopambana kuhakikisha Trump apitishwi kugombea uraisi kwa tikei ya Republican ni aliyekua mgombea wa uraisi 2014 Mitt Romney. Romney ambaye aligombea uraisi na Barack obama anamshutumu Trump kwa ubadhilifu, ubaguzi na chuki dhidi ya wanawake, 

Trump anasema akiwa raisi atajenga ukuta mkubwa katika mpaka wa Marekani na Mexico ili kuhakikisha watu hao awaingii nchini kwake. 

Pia inasemekani kwamba Trump anatoa harufu ya chuki dhidi ya dini, bilionea huyo alisema ataki waislamu waingie Marekani, hoja yake ikiwa watu hao wamekua wakisababisha matukio ya kigaidi yanayotokea nchini humo. 

Kauli nyingine tata ndio zinawafanya wakina Romney na viongozi wengine kupambana ili asipite kugombea uraisi kwa hofu kwamba Marekani itakua kwenye mikono mibaya chini yake. Pia Trump alikaririwa akisema kwamba mikataba mibaya dhidi ya China na Mexico ndio sababisho la kuzorota uchumi wa marekani na uzalishaji mbovu wa ajira. 

Alihaidi kufanya mikataba na mataifa mengine itakayo walinda wafanyakazi wa marekani na ametishia kupandisha kodi kwa bidhaa zote zinazoingia marekani kutoka nje ili kuinua uzalishaji wa ndani. 

Image result for us election donald trump

Mikataba inayotajwa kuwanufaisha wafanya biashara wakubwa na kuwanyima ajira na kipato wamarekani ni kama ule wa makubaliano ya biashara huru nchi za Amerika Kaskazini au North America Free trade agreement (nafta) uliotiwa saini na rais Bill Clinton.

Kwa mujibu wa wachunguzi wa biashara za kiuchumi, miaka kumi ya nafta, wamarekani 766,000 wamkeosa ajira baada ya wamiliki wa viwanda kufungua viwanda nchi za Canada na Mexico badala ya Marekani.

Ijulikani kwamba Hillary Clinton anawania uraisi kwa tiketi ya Democrats. 

Image result for us election donald trump

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.