MAN CITY, CHELSEA ZASHINDA LIVERPOOL YATOKA SARE.


Manchester City imepanda hadi nafasi ya tatu katika jedwali la ligi ya Uingereza baada ya kuicharaza Stoke City 4-0 huku ikitarajiwa kumenyana ana Real Madrid katika kombe la vilabu bingwa Ulaya siku ya Jumanne.
Fernando alifunga kwa kichwa na kuwaweka City kifua mbele kabla ya Sergio Aguerro kufunga kwa njia ya Penalti.

Baadaye Kelechi Ihienacho aliyetangazwa mchezaji bora katika mechi hiyo alifunga mabao mawili.
Kwengineko Eden Hazard alifunga bao lake la kwanza na kuisadia timu yake kuishinda Bournemouth.

Cesc Fabregas alisaidia katika mabao matatu ya Chelsea akitoa pasi nzuri kwa wafungaji Pedro,Hazard na baadaye Willian.
Vilevile Newcastle iliimarisha matumaini yao ya kusalia katika ligi ya Uingereza baada ya kutoka sare ya 2-2 na wenyeji Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Daniel Sturridge na Adam Lalana waliiweka mbele Liverpool kabla ya Newcastle kukomboa kupitia Papis Cisse na Colback 

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.