MANCHESTER UNITED, YAWEKA REKODI KOMBE LA FA.





Bao la lala salama la Antony Martial limeipa rekodi Manchester United kucheza fainali ya 19 ya FA Cup kufuatia ushindi wa Everton kwenye uwanja wa Wembley.
Martial alikihakikishia ushindi kikosi cha Louis van Gaal ambacho sasa kitakutana na Crystal Palace au Watford kwenye mchezo wa fainali.
Marouane Fellaini aliifungia United bao la kuiongoza kwa shuti la karibu lakini shukrani za United zinakwenda kwa David de Gea aliyeokoa penati ya Romelu Lukaku dakika ya 57.
Everton walipata bao lao la kusawazisha zikiwa zimesalia dakika 15 mchezo kumalizika ambapo Chris Smalling alijifunga wakati akijaribu kuokoa mpira wa krosi ya Gerard Deulofeu.
Wakati mchezo ukionekana utakwenda kwenye dakika za nyongeza, Ander Herrera alipiga pasi iliyomkuta Martial ambaye aliupachika mpira kambani huku golikipa waEvertton Joel Robles asijue cha kufanya.
YAFAHAMU HAYA.....
  • Marouane Fellaini amefunga magoli mawili kwenye mechi tano za FA Cup alizocheza msimu huu huku akiwa na goli moja kwenye ligi katika mechi 17 alizocheza.
  • Assists saba za Anthony Martial kwenye msimu huu, nne kati ya hizo zinatoka kwenye michuano FA Cup.
  • Romelu Lukaku amekosa mikwaju miwili ya penati katika mechi mbili zilizopita akiichezea Everton baada ya kuifunga mikwaju mingine mitano ya penati katika mechi zilizopita (kwenye mashindano yote.)
  • Chris Smalling amejifunga kwa mara ya kwanza (mashindano yote) tangu alipofanya hivyo kwa mara mwisho mwaka 2010, ikiwa dhidi ya Everton wakati akiichezea Fulham.
  • Martial ame-assist na kufunga goli kwenye mechi moja kwa mara ya tatu sasa msimu huu.
  • Martial amehusika kwenye magoli 21 ya United msimu huu, akiwa amefunga magoli 14 na ku-assist mengine saba kwenye mashindano yote.
  • United wanafanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya FA Cup kwa mara ya kwanza tangu 2007.
  • Everton wametupwa nje ya FA Cup katika hatua ya nufu fainali mara mbili mfululizo baada ya kufanikiwa kuika hatua hiyo, kabla ya kuchapwa na United walipoteza mbele ya Liverpool mwaka 2012.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.