MASHABIKI WA LIVERPOOL WAIFURAHIA RATIBA YA NUSU FAINALI UEFA 2016.
SPORTS.
MASHABIKI WA LIVERPOOL WANAFURAHIA RATIBA YA NUSU FAINALI EUROPA LEAGUE
By Justin Mario on 15 April 2016
Baada ya raiba ya UEFA Champions League kutoka, ratiba ya Europa League pia nayo imewekwa hadharani ambapo michezo ya miwili ya raundi ya kwanza nay a pili imepangwa kupigwa April 28 na May 5.
Wakiwa na furaha ya matokeo ya matokeo ya ushindi wa kukumbukwa dhidi ya Borussia Dortmund, Liverpool imepangwa na Villarreal katika mchezo wake wa nusu fainali.
Manyambizi hao wa njano kutoka Hispania wanakamatia nafasi ya nne kwenye msimamo wa La Liga hawajawahi kukutana na Liverpool hata mara moja kwenye historia lakini watakuwa na wakati mgumu kutokana na mchezo wao wa marudiano kupigwa kwenye dimba la Anfield.
Mashabiki wa Liverpool wamefurahishwa na ratiba hiyo kutokana na kuwakwepa mabingwa watetezi Europa League klabu ya Sevilla pamoja na wakali wengine wa Ukraine, Shakhtar Donetsk.
Kufuatia ushindi wa usiku uliopita, mashabiki wa Liverpool wamefurahishwa sana na ratiba hiyo pale walipojua kuwa game ya marudiano itafanyikia kwenye uwanja wa Anfield. Sehemu ngumu kutoka na ushindi bila kujali matokeo ya mchezo wa kwanza yalikuwaje.
No comments:
Post a Comment