SAFARI YA KWANZA YA NJE YA MH. RAIS MAGUFULI KESHO.....
MH. Dk John Pombe Magufuli, April 5 2016 kakukubali mwaliko wa Rais Paul Kagame wa Rwanda, hivyo atafanya ziara ya siku mbili Jumatano na Alhamisi.
Stori kutoka wizara ya mambo ya nje zinaeleza kuwa Rais Magufuli pamoja na Rais Kagame watafungua daraja la kimataifa la Rusumo linaounganisha mpaka wa Tanzaniana Rwanda na kuzindua huduma za kituo cha pamoja. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari na kusomwa katika television za Tanzania Rais Magufuli atasafiri kwa gari.
Rais Magufuli pia atakwenda kuweka shada katika makaburi ya mauaji ya Kimbali ya mwaka 1994 na baadae kufanya mazungumzo ya pamoja na Rais Kagame mjini Kigali. Hii ndio itakuwa safari ya kwanza ya Rais Magufuli kusafiri nje ya nchi toka aingie madarakani October 2015.
No comments:
Post a Comment