SERIKALI YA UGANDA YAMKABA EX- WA ZARI, ( IVAN ), SABABU HII HAPA...
Mfanya biashara maarufu kutoka Uganda anayeishi Afrika Kusini Ivan Ssemwanga ameingia kwenye skendo kubwa na Idara ya Maji ya nchini Uganda baada ya kukutwa na maji yaliyoonganishwa kwa wizi nyumbani kwake.
Uganda National Water and Sewerage Cooperation imesema Ivan anatumia maji yaliyovutwa nyumbani kwake kinyume cha Sheria.
Ivan ni CEO Wa kundi la Uganda la Rich Gang, anatumia maji ya uwizi kwenye nyumba yake huko Muyenga mjini Kampala.
Ivan Alitoa mita ya maji miezi kadha nyuma na ameacha kulipa bili yake ya maji.
Ivan amejipatia umaarufu mkubwa Afrika Mashariki baad aya Zari kuanza kutoka na Diamond Platnumz, Zari amezaa watoto watatu na Ivan.
No comments:
Post a Comment