MATCH PREVIEW : UEFA SEMI FINAL - A. MADRID VS BAYERN 27/04
Macho yote ya wapenda soka duniani yatakuwa kwenye dimba la Vicente Calderon usiku wa leo kushuhudia pambano la nusu fainali ya Champions League kati ya wenyeji Atletico Madrid dhidi ya Bayern Munich.
Baada ya Atletico kuisukuma Barcelona nje ya mashindano kwenye hatua ya robo fainali, ni vigumu kutabiri nini kitatokea katika mchezo huo ambapo kikosi cha Diego Simeone kitakuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Bayern Munich wenye safu bora ya ushambuliaji kwenye michuano hiyo wakiwa wameshazamisha goli 28 wavuni hadi sasa katika campaign za kuhakikisha wanabeba ndoo ya UEFA msimu huu.
Robert Lewandowski na Thomas Muller kwa pamoja wamefunga magoli 16 kwenye michuano ya Champions League msimu huu, mabao mengi zaidi kuliko ya Atletico.
Bayern pia wanahistoria na uzoefu pia kwenye kikosi chao. Hii ni mara ya 17 kwa The Bavarians kufika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya . tofauti na Atletico Madrid ambao wametinga hatua ya nne bora mara tatu katika misimu tofauti.
Kwa kifupi, Bayern wanapewa nafasi kubwa ya kushinda pambano la leo lakini kiuhalisia pambano linaweza kumalizika tofauti na hivyo.
Atletico watamkosa beki wao wa kati Diego Godin, Fernando Torres atarejea kikosini baada ya kufunga magoli matano kwenye mechi sita. Anatarajia kuanza na partner wake Antoine Griezmann kwenye safu ya ushambulizi, Mfaransa huyo tayari amefunga magoli 20 kwenye La Liga msimu huu.
Atletico watakuwa na uhakika wa kuweka rekodi kwenye usiku wa leo, The Rojiblancos wameshinda michezo 12 kati ya mechi 16 za Champions League kwenye uwanja wa Calderon chini ya Diego Simeone na hawajaruhusu goli kwenye michezo 13 kati ya 15 ilyopita.
Bayern wao watamkosa Arjen Robben lakini wanapata nguvu kutokana na kurejea kwa mlinzi wao wa kati Jerome Boateng kwa mara ya kwanza baada ya kukaa nje ya uwanja kwa miezi mitatu.
Kikosi cha Atletico Madrid kinachotarajiwa kuwanza kwenye mchezo wa leo
Kikosi cha Bayern Munich kitakachoikabili Atletico kwenye mchezo wa leo usiku
No comments:
Post a Comment