UNATAKA KUFUFUA MAHUSIANO YAKO YANAYOKARIBIA KUFA?? MBINU HIZI HAPA



Mapenzi ni hisia zinazoumiza lakini hazichoshi, hata uumizwe vipi huwezi kuacha kupenda, na katika maisha, mapenzi yana nafasi kubwa sana

Tazama vikwazo,
Ni muhimu kujua nini vikwazo vilivyosababisha penzi lenu kuisha na jitahidi kutatua hivyo vikwazo maana bila kufanya hivyo hautofanikiwa kufufua mahusiano yako.

Amua kumpenda kama zamani,
Inabidi kutoka ndani ya moyo ukubali kumpenda kwa dhati na kumuonyesha mapenzi ambayo hapo nyuma hukuwahi kumuonyesha.

Omba msamaha.
Kubali kuomba msamaha hata kama kosa halikuwa lako kubali kujishusha kwasababu wewe ndiye unaetaka mapenzi yenu yawe kama zamani.

Kurejesha mawasiliano,
Jitahidi kuboresha mawasiliano haswa mkiwa mbali ili kuweza kuleta ukaribu, kujua yuko wapi anafanya nini na nani.

Uaminifu,
Muamini kwa lolote atakalokwambia na usimfanye ahisi kwamba humuamini kwa sababu hiyo itasababisha kukukwepa msiwe mnaonana

Mazungumzo,
Ni muhimu kumkumbushia maisha ya zamani mliyopitia kipindi cha furaha na epuka kumkumbushia mabaya mliyowahi kufanyiana  kipindi cha nyuma.

Msifie,
Mfanye ajione kwamba yeye ni mzuri au handsome kwamba hujawahi kupenda kama unavyompenda yeye pia ajue kwamba yeye ndo kitu bora zaidi katika maisha yako.

Zawadi,
Mnunulie zawadi tofauti na sio lazima hizo zawadi ziwe za gharama ya juu hata vitu vidogo vidogo vinaweza kuwa zawadi na mpenzi wako akafurahi.

Tenga muda kwa ajili yake,
Kutenga muda wa kumuuliza mambo yanayomuhusu yeye na hii itakusaidia wewe kujua wapi unafanya sahihi na wapi unakosea.


No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.