PICHA : WATU 32 WAPOTEZA MAISHA BAAADA YA NDEGE KUPATA AJALI NA KUANGUKIA NYUMBA ZA WATU



Watu zaidi ya 32 wamefariki baada ya ndege ya kubeba mizigo ya Uturuki, iliyokuwa safarini kutoka Hong Kong kuangukia nyumba za watu karibu na mji wa Bishkek nchini Kyrgyzstan.

Taarifa zinasema wengi wa waliokufa ni watu waliokuwa ardhini, ndege hiyo aina ya Boeing 747 ilianguka karibu na uwanja wa ndege wa Manas, takriban kilomita 25 kutoka mji mkuu Bishkek,

Nyumba zaidi ya 15 zimeharibiwa na watoto kadha wanaripotiwa kuwa miongoni mwa waliofariki. Imeelezwa kuwa hali ya hewa ilikuwa mbaya na kulikuwa na ukungu, ingawa chanzo hasa cha ajali hiyo hakijathibitishwa.






No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.