ATLETICO MADRID YANG'AA NUSU FAINALI YA PILI - UEFA, ANGALIA HAPA JINSI ILIVYOKUA MECHI HIYO ( VIDEO )










April 27 2016 nusu fainali ya pili ya michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya iliendelea, baada ya Jumanne ya April 26 kushuhudia mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Klabu Bingwa Ulaya iliyokuwa inazihusisha timu za Man City dhidi ya Real Madrid na mchezo kumalizika kwa sare ya 0-0.
Jumatano ya April 27 katika uwanja wa Atletico Madrid Hispania unaojulikana kwa jina la Calderon, ulipigwa mchezo wa pili uliokutanisha wenyeji wa uwanja huo dhidi ya FC Bayern, hadi dakika 90 zinamalizika Atletico Madrid walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa dakika ya 11 na Niguez Esclape.
1836
Licha ya kuwa Atletico Madrid wameibuka na ushindi huo, FC Bayern walikuwa wanamiliki mpira kwa asilimia 70 na wenyeji wao asilimia 30, kitu ambacho kitawapa tabu mchezo wa marudiano, Atletico watapata shida na ukilinganisha na rekodi ya FC Bayern ya kupenda kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa.
Video ya magoli ya Atletico Madrid 1 – 0 Bayern Munich

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.