50 CENT AOMBA RADHI KWA HILI...



4 May 2016

Lejendari wa Muziki wa HipHop nchini Marekani anayesifika kwa matukio ya kibabe 50 Cent hivi karibuni amefanya tukio la kidhalilishaji kwa mfanyakazi wa Uwanja wa Ndege mwenye ulemavu na kuibua hisia tofauti kwa wanajamii.

Taarifa kutoka katika mtandao wa TMZ zinasema 50 Cent alichukua video na kuituma kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha kijana Andrew ambaye ni mlemavu wa viungo na kutosikia akiwa katika majukumu yake ya kazi huku 50 akimkejeli kwamba kijana huyo amelewa.

Baada ya tukio hilo msanii 50 Cent amesema tayari ameomba radhi kwa kijana huyo pamoja na familia yake kwani hakukusudia kufanya kitendo hicho.

Hata hivyo familia ya kijana huyo ilikuwa tayari kumchukulia hatua za kisheria 50 Cent kutokana na kitendo hicho cha kidhalilishaji.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.