ZINEDINE ZIDANE AMEYASEMA HAYA KUELEKEA FAINALI YA UEFA LEO
Boss wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema kupoteza mchezo wa fainali ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid haimaanishi kwamba amefeli.
Real Madrid maarufu kama Los Blancos wataingia kwenye fainali ya Jumamosi dhidi ya mahasimu wao wa jiji moja wakiwa hatarini kumaliza msimu mikono mitupu kama watashindwa kutwaa taji hilo la Ulaya.
Wamemaliza katika nafasi ya pili katika La Liga nyuma ya mabingwa FC Barcelona huku wakiwa tayari wamelikosa pia kombe la Copa del Rey baada ya kutupwa nje kwa kumchezesha mchezaji asiyestahili Denis Cheryshev licha ya ushindi wao wa magoli 3-1 dhidi ya Cadiz mwezi December mwaka uliopita.
Zidane alichukua nafasi ya Rafael Benitez mwezi January, amesisitiza kwamba, kufungwa kwenye mchezo wao wa fainali haitachukuliwa kama wamefeli baada ya kupambana na hatimaye kufanikiwa kufika San Siro.
Nyota huyo wa zamani wa Madrid amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari: “ Sidhani kama itakuwa tumefeli kama tutapoteza mchezo wa fainali, hakuna atakayebeza tulichokifanya hadi tumefika hapa.”
“Kushindwa kutakuja pale tutakaposhindwa kuheshimu kazi tuliyoifanya huko nyuma hadi leo tuko hapa, lakini tukumbuke huu ni mchezo wa soka.”
“Hakuna anayejua nini kitatokea. Ninachowezakusema ni kwamba tukotayari kwa ajili ya mchezo. Bado mchezo mmoja pekee. Tunafurahi kuwa kwenye fanali hii na neno pekee ni kwamba tuko tayari kwa lolote.”
“Nimefanya kazi kubwa pamoja na wachezaji wote na tunastahili kuwa hapa. Tumepambana sana lakini hiyo ni kawaida. Bila kupambana ni vigumu kufika hatua ya fainali.”
Madrid wamefunga magoli mengi pengine mara mbili zaidi ya yale ya Atletico Madrid kwenye mashindano ya Champions League msimu huu, wamefunga magoli 27 wakati Atletico Madrid wao wakiwa wamefunga magoli 16.
Madrid iliifunga Atletico 4-1 kwenye fainali ya mwaka 2014 baada ya Sergio Ramos kusawazisha bao dakika za lala salama na kuufanya mchezo kwenda hadi extra time na Atletico kuruhusu Gareth Bale, Marcelo and Cristiano Ronaldo kutikisa nyavu nao na kutwaa ubingwa.
Zidane anataka kurudia matokeo kama hayo licha ya kikosi chake kuwakosa Iker Casillas na Sami Khedira wakali waliokuwepo kwenye mchezo wa mwaka 2014 lakini tayari walishaondoka kwenye kikosi hicho lakini bado hakijayumba.
Amesema: “Baadhi ya wachezaji hawapo tena kwenye klabu lakini falsafa yetu inabaki palepale. Lengo la Real Madrid limekuwa ni kutengeneza historia kubwa kwaajili ya klabu, kuungana pamoja, kufanya kazi kwa pamoja, kucheza kwa ubora na kucheza katika kiwango kwenye kila mechi.”
“Tunachotaka kufanya kesho ni kurudia kile tulichofanya 2014 na kufanya chochote tutakachoweza kuhakikisha tunashinda mchezo huo.”
Aliongeza: “Ninahakika wakati mchezo unaanza kidogo nitakuwa na presha kama kawaida lakini naipenda kazi hii. Napenda presha, nimeshaishi kama mchezaji na unapokuwa kocha ni tofauti kabisa.”
“Carlo Ancelotti alinimbia hivyo mara nyingi. Alinimbia hivyo kabla ya mchezo wa Lisbon (mwaka 2014), ‘Namini sikumoja utaishi maisha ya ukocha’ na ndivyo ilivyo sasa.”
No comments:
Post a Comment