ENGLAND, WALES MBELE MICHUANO YA EURO 2016


Wales ilijifurukuta na kuilaza Urusi mabao matatu kwa nunge katika mechi ya mwisho na muhimu ya makundi jana usiku.
Aaron Ramsey na Neil Taylor na Gareth Bale walifunga mabao hayo muhimu na kuisaidia timu hiyo ya kocha Chris Coleman ikiwa imejihakikishia nafasi katika mkumbo wa pili kwa mara ya pili katika historia yake.
Wapinzani wao wa jadi England walimudu sare tasa dhidi ya Slovakia mjini Saint-Etienne na kuhakikisha kuwa Wales wanafuzu kwa raundi ya pili ya mashindano hayo kama vinara wa kundi B.
Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Wales sasa watachuana na mshindi wa tatu katika kundi C A ama D.
Wales na England zimefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Euro baada ya mechi zake za kundi B kukamilika.
Vijana wa Chris Coleman wamewabamiza Russia mabao 3 kwa 0 na huku England ikija ya pili kwenye kundi baada ya kubanwa mbavu na Slovakia.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.