HONG KONG NDIO MJI GHALI ZAIDI DUNIANI

Hong Kong


Mji wa Hong Kong ndio mji ghali zaidi duniani baada ya kuupiku mji wa Luanda, Angola kulingana na wafanyikazi wa kimataifa katika utafiti wa kila mwaka unaofanywa na shirika la Mercer.

Luanda ambao ulikuwa unaongoza orodha hiyo katika siku za hivi karibuni ulishuka kufuatia kudhoofika kwa sarufi yake.

Mji wa Luanda


Mji wa Zurich na Singapore ni ya tatu na nne mtawalia katika orodha hiyo ikiwa haijabadilika kwa mwaka mmoja sasa.

Mji wa Zurich
Singapore
Mji wa Tokyo sasa umepanda hadi nafasi ya tano.

Tokyo


Utafiti huo unalenga kampuni zinazotakiwa kuhesabu marupurupu ya wafanyikazi wa kimataifa.


Umepima gharama ya kuishi kwa takriban mataifa 209 duniani,ikilinganisha gharama ya viti 200 katika kila eneo ikiwemo,bei ya nyumba ya kuishi,uchukuzi,chakula na burudani.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.