SHEREHE ZA KULA NYAMA YA MBWA CHINA

raia wakifurahia nyama ya mbwa China


Sherehe ya kila mwaka ya kula mbwa imeanza kusini mwa taifa la China licha ya pingamizi kutoka katika taifa hilo na ugenini

Takriban mbwa 10,000 na paka wanatarajiwa kuuawa na kuliwa wakati wa sherehe hiyo ya siku kumi inayofanyika Yulin.

Wanaharakati wanasema kuwa hafla hiyo ina ukatili huku wale wanaotaka sherehe hiyo kupigwa marufuku wakiandikisha saini milioni 11.



Mamlaka ya eneo hilo inasema kuwa sherehe hiyo haiungwi mkono moja kwa moja na serikali lakini hufanywa na wafanyibiashara wa kibinafsi.

Je,sherehe hiyo inahusu nini?
Sherehe hiyo ya mlo wa nyama ya mbwa huwaleta pamoja watu wengi katika eneo la Yulin ili kujichagulia nyama ya mbwa, matunda na vinywaji.

sherehe zya nyama ya mbwa Yulin

Utamaduni wa kula nyama ya mbwa ulianza miaka 500 iliopita nchini China,Korea Kusini pamoja na mataifa mengine ambapo wengi wanaamini mlo huo huondoa joto mwilini wakati wa majira ya kiangazi.






No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.