IDRISSA SULTAN NAYE AUNGANA NA JUSTIN BIEBER KWA KUFUTA ACCOUNT YAKE YA INSTAGRAM PIA



Hivi karibuni kuliibuka tetesi za staa huyo kumwagana na mpenzi wake Wema Sepetu huku chanzo cha ugomvi huo ikitajwa ni kuchoshwa na tabia ya mpenzi wake huyo kutompa support kwenye show zake.
Mashabiki wa Wema Sepetu wa mitandaoni maarufu kama ‘Team Wema’ waliibuka na kuanza kumtukana Idris hata hivyo staa huyo alivunja ukimya kwa kutoa yaliyokuwa moyoni kwenye mtandao wake wa instagram, aliandika:
“Sipendi kuona watu wakiingia na kuongea kama wanajua maisha yangu na watu wangu wa karibu, makosa wakifanya wengine mnakuja kwangu mnaanza “Ndio asingefanya vile kama sio wewe kufanya hivi” mnakazana kusema eti naposti wanawake mara ooo porojo kibao. Sina freedom ya kumpost dada angu ? Kweli ? Au rafiki yangu kazindua brand mpya siwezi mpost nikampongeza?.”
“Mnauliza kwanini sijaenda vigoma nimesema because show yangu hakuja hata moja na nimeenda show zake zote na yeye halalamiki because anajua nimesema siendi fair enough mbona hamjaongelea hilo? I repeat nikikaa kimya is for a pure reason that it’s not anyones business this is my personal life kama mnaongeleaga fair basi mngefanya kuuliza kwanini mpaka am selling out hajaja,” aliongeza.
“Give me a break sina maisha ya kuigiza lets have respect for each other bana. Na nimesema msiniite shemeji for one big good reason, imekua too much i am a brand na jina idris linamezwa na shem, ningejua this from the beginning nisingeruhusu mniite tangu mwanzo so msiwe kila kitu mnafikiria negative tu. Na sikuwa na haja ya kuandika yote haya pia Tusichukuliane Poa.”
Kenya 1
Hata hivyo Jumatatu ya wiki hii Wema naye alimpigilia msumari wa moto Idris kwa kupost picha ya wanaume anaowapenda #MCM (Man Crush Monday) na mmoja wao akiwa Diamond.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.