BREAKING NEWS : WANAWAKE WALIOVALIA MABUIBUI WAFANYA SHAMBULIO LA KIGAIDI HUKO MOMBASA, NCHINI KENYA

Image result for breaking news

Wanawake watano waliovalia mabuibui na walioaminika kuvaa mikanda ya kujilipua walivamia kituo kimoja cha polisi mjini Mombasa katika shambulio la kigaidi.
Maafisa wa polisi nchini Mombasa wanasema kuwa walitibua jaribio hilo na kufanikiwa kuwaua wanawake watatu huku wawili wakikamatwa.
Polisi wanasema kuwa washukiwa hao waliwasili katika kituo cha polisi cha Central ili kuripoti kuhusu simu ilioibiwa.
Na wakati malalamishi yao yalipokuwa yakichukuliwa mmoja wao alichukua kisu na kuwadunga maafisa wawili wa polisi ,huku mwengine akiwarushia polisi waliokuwa wakichukua malamishi hayo bomu la petroli.
Polisi wanasema kuwa waliwafyatulia risasi na kuwaua wote.
Maafisa waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini huku kituo hicho cha polisi kikilindwa ili kuhakikisha kuwa hakuna tishio jingine.
Kumekuwa na mashambulio kadhaa katika eneo la pwani ya Kenya katika miaka ya hivi karibuni mengi yakifanywa na kundi la kigaidi la al-Shabab.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.