FRIDAY XO : MICHEPUKO KWENYE MAHUSIANO YA KIMAPENZI, NANI WA KULAUMIWA?
Mara kwa mara nimewasikia watu wakisema hivi : asili ya mwanaume kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja na nimekuwa nikijiuliza maana yake; nimeishia na tafsiri kwamba wanawake ni waaminifu na huwa na mpenzi mmoja tu na wanaume sio waaminifu hata kidogo.
Ni ukweli usiofichika kwamba ni rahisi zaidi kwa mwanaume kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja ingawa sisemi kwamba wanawake hawana tabia ya kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja au kutoka nje ya ndoa lakini mara nyingi zaidi uaminifu unakosekana kwa wanaume iwe katika mahusiano ya kimapenzi au ndoa.
Wanawake pia wanakosa uaminifu wakati mwingine, wanawake wana sababu zao na wanaume pia wana sababu za kukosa uaminifu katika mahusiano, lakini hakuna sababu ya aina yoyote inalofanya hili kuwa sahihi.
Wanaume wanakuwa na wapenzi wengi kwa sababu wanavyofikiria ngono…? Ni tofauti na wanawake, hawaichukulii kwa dhati kama wanaume.
Mwanaume anaweza kulala na mwanamke yeyote wakati wowote na asijutie kwani baada ya tendo hilo yeye anaweza kuondoka na kuendelea na maisha yake kama vile hakuna kilichotokea.
Hii ni tofauti kabisa kwa wanawake ambao wanachukulia kujamiiana kuwa ni tendo muhimu na la kisiri sana katika mahusiano wanayokuwa nayo, wanaona ngono ni jinsi ya kuonesha mapenzi na hisia zao kwa wapenzi wao, hii ikiwa na tafsiri kwamba mwanamke hawezi kulala na mtu asiyempenda.
Hata kama mwanaume anampenda mpenzi wake kiasi gani, si rahisi sana kuwa muaminifu kwake, mwanaume ana shauku ya kutaka kujaribu kitu kipya kila wakati, kama jogoo anavyopenda kujaribu kila kuku anayemuona.
Hata mpenzi wake amridhishe vipi, bado atakwenda kutafuta kitu kipya, cha ajabu ni kwamba yeye anakwenda kwa sababu ya ngono tu na si kitu kingine, hakuna hisia anazokuwa nazo kwa wanawake wengine kwa sababu upendo wake wote anampa mwanamke mmoja tu.
Kila mtu ana malengo katika maisha yake, wote tuna ndoto za kufika mahali fulani, au kufanya kazi fulani, wanaume wanakuwa na ari zaidi katika hili, hii ni kwa sababu mwanaume asipopata kile anachotaka, basi atavipa kipaumbele anapotaka.
No comments:
Post a Comment